Posted on: March 2024
Wanufaika wa Mradi wa FOSENI II (Uhakika wa Chakula na Uboreshaji wa Lishe), unatekelezwa na Integrated Rural Development Organization (IRDO) katika vijiji 11 vya Wilaya ya Ileje, Mkoa wa Songwe, wamekabidhiwa kuku kwa ajili ya kufuga kama sehemu ya kuwawezesha kiuchumi na kuboresha hali ya lishe katika kaya zao.
Kuku hao walikabidhiwa rasmi na Mratibu wa Mradi, Bw. Gaster Kihwello, akiwaeleza wanufaika kuwa ufugaji huo utawasaidia kujiongezea kipato kupitia uuzaji wa mayai na kuku pamoja na kuboresha lishe ya familia kwa kutumia mayai na nyama ya kuku.
Kupitia mradi huu, IRDO inaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kupambana na udumavu, kuboresha usalama wa chakula, na kuongeza kipato cha kaya kupitia shughuli endelevu za ufugaji.